IQNA

Mufti wa Misri ataka kuundwa Jumuiya ya kimataifa ya Waislamu waliowachache

17:11 - March 04, 2009
Habari ID: 1751838
Mufti wa Misri ametoa wito wa kuasisiwa jumuiya ya kimataifa itakayoshughulikia masuala ya Waislamu katika nchi na maeneo wanakokuwa wachache. Ali Juma aliyasema hayo mjini Cairo katika mazungumzo yake na balozi wa Thailand nchini Misri.
Mufti wa Misri amesema kuwa jumuiya hiyo inapaswa kuwashirikisha wawakilishi wa Waislamu wanaokuwa wachache katika nchi au maeneo yao kote duniani kwa lengo ya kushughulikia masuala ya Waislamu kwenye maeneo hayo.
Amesisitiza kuwa jumuiya hiyo itawasaidia Waislamu wanaoishi katika maeneowanapokuwa jamii ya wachache na kutatua kisheria matatizo yao mbalimbali katika jamii zisizokuwa za Kiislamu.
Ali Juma ameongeza kuwa jumuiya hiyo itakuwa daraja ya mawasiliano ya kuwakurubisha Waislamu wanaoishi katika jamii zisizokuwa za Kiislamu na taasisi rasmi, jumuiya za Kiislamu na taasisi za kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu. 372255
captcha