Semina hiyo ilianza mapema asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Istiqlal mjini Tehran ikiwashirikisha wanasheria, majaji, mawakili na wahadhiri wa vyuo vikuu.
Mkutano huo uliojadili kadhia ya Palestina na ukiukwaji mkubwa wa haki za bindamu unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, ulikuwa utangulizi wa mkutano wa kimataifa wa kuwaunga mkono wananchi wa Gaza ulioanza kazi zake leo mjini Tehran. Habari zaidi kuhusu mkutano wa leo zitakujieni baadaye. 372285