Akizungumza hivi karibuni mbele ya wanazuoni wa Kishia na Kisuni huko katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, Hujjatul Islam wal Muslimeen Mustafa Pur Muhammadi amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaoeneza propaganda chafu na fitina ulimwenguni kwamba Iran inataka kueneza fikra za Ushia duniani. Amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasaidia ndugu zake wa Kiafghani katika mazingira magumu na kwamba kwa muda wa miaka 30 sasa imekuwa ikiwapa hifadhi wakimbizi wa nchi hiyo.
Mustafa Pur Muhammadi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 47 Iran imekuwa ikitetea na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika mazingira magumu sana na kwamba hadi sasa imelipa gharama kubwa kwa kuwatetea wanamapambano wa Ukanda wa Gaza, hali ya kuwa Waislamu wa nchi mbili hizo sio wafuasi wa madhehebu ya Shia. Amesema jambo lililo na umuhimu katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa ni kuimarishwa muamko na utukufu wa Kiislamu. Amesema, wimbi la muamko wa Kiislamu linaloshuhudiwa katika pembe mbalimbali za dunia linatokana na baraka za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Amewataka wanazuoni kuwa katika mstari wa mbele wa kutatua matatizo ya jamii na ya ulimwengu wa Kiislamu na kutokwepa majukumu hayo na kuwatupia viongozi wa serikali. 373105