IQNA

Nchi za Kiislamu zifanye juhudi za kuimarisha nafasi ya wanawake

18:33 - March 10, 2009
Habari ID: 1754497
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Isesco limetoa taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Wanawake Duniani likizitaka nchi za Kiislamu kufanya juhudi za kuboresha hali ya wanawake na kuzidisha mchango wao katika nyanja za kijamii na kiuchumi.
Taarifa hiyo imesisitiza juu ya kuimarishwa nafasi ya kielimu ya wanawake wa Kiislamu ili kuimarisha mchango wao katika jamii.
Shirika hilo limezitaka taasisi za serikali na zisizo za serikali za nchi za Kiislamu kufanya juhudi maradufu za kuwashirikisha zaidi wanawake katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Taarifa hiyo inasema kuwa kwa kutilia maanani kwamba Uislamu ni dini ya uadilifu, kila juhudi zinapasa kufanywa ili kulinda haki zote za wanawame.
Kuandaliwa kikao cha masomo maalumu kwa mabinti na wanawake wa Kiislamu nchini Yemen na kingine cha wanawake wabunifu nchini Tunisia ni miongoni mwa juhudi ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Isesco kwa ajili ya kunyanyua nafasi ya wanawake wa Kiislamu katika jamii. Shirika hilo pia lilishiriki vilivyo katika kikao cha kimataifa cha haki za wanawake kilichofanyika mjini Tehran mwezi Septemba mwaka uliopita. 375232
captcha