Kwa mujibu wa tovuti ya Islam online, Sheikh King Amba, mtaalamu wa masuala ya kidini na mmoja wa wanachama wa kamati iliyoandaa sherehe hizo amesema katika mahojiano na shirika la habari la IQNA kuwa, viongozi wa Kikristo walioshiriki katika sherehe hizo wamekaribisha suala hilo wakisema kuwa bila shaka litawasaidia kuelewa vyema dini ya Kiislamu.
Sheikh Amba amesema, mwaliko huo kwa Wakristo unatokana na mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw) ya kuwasihi wafuasi wake waishi pamoja kwa amani, umoja na usamehevu na wafuasi wa dini nyinginezo.
Huku akidhihirisha furaha yake kutokana na mwaliko huo wa Waislamu, Askofu George Bulya wa Kanisa Katoliki nchini Malawi amesema kuwa, kualikwa Wakrsito katika sherehe hizo kutasaidia mno katika kuondoa baadhi ya imani potofu iliyoko miongoni mwa Wakristo kuhuisiana na Uislamu na Waislamu.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Malawi, Waislamu wanaunda asilimia 12 ya jamii ya nchi hiyo. Uislamu ndiyo dini iliyo na wafuasi wengi zaidi nchini humo baada ya Ukristo. 375904