Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo imesema kuwa inasikitisha kwamba kwa mara nyingine tena tumeshuhudia jinai za utumiaji mabavu na ukatili wa kundi lenye chuki za kimadhehebu tena katika mji mtakatifu wa Madina na kandokando ya haram ya Mtume Mtukufu. Vitendo hivyo viovu vinafanywa na kundi dogo ambalo linachafua sura safi ya Uislamu.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema kuwa matendo machafu ya kundi linalowapiga, kuwajeruhi na kuwaua Waislamu kwa kisingizio cha kuamrisha mema na kukataza maovu ni kielelezo halisi cha maovu. Kundi hilo ndilo lililonyamaza kimya mbele ya jinai kubwa zaidi katika historia ya mwanadamu yaani jinai za utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, bali hata kuunga jinai hizo kwa njia mbalimbali.
Taarifa ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kidini cha Shiraz imeeleza mshikamano wake na Waislamu wa Kishia wanaokandamizwa nchini Saudi Arabia hususan katika maeneo ya Ihsaa na Qatif, na kuzitaka jamii za Kiislamu na wanafikra Waislamu kuzuia vitendo hivyo viovu. Vilevile imeitaka Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatilia suala hilo kupitia taasisi za kimataifa na njia za kidiplomasia.
Hivi karibuni polisi ya Saudi Arabia iliwashambulia na kuwapiga Waislamau wa madhebu ya Shia waliokuwa wakifanya ziara karibu na msikiti wa Mtume Muhammad mjini Madina na kuwatia nguvuni baadhi yao. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa Waislamu mawili waliuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na kundi la Mawahabi kwa kutumia kisingizio cha kukataza mauvu na wengine wamelazwa mahospitalini. 375795