Ban Ki- moon amewaandikia baria washiriki wa kikao cha Umoja wa Mataifa kinachoendelea nchini Misri kuhusiana na Ukanda wa Gaza na kusisitiza kwamba, kivuko cha Rafah kinapasa kufunguliwa mara moja na usitishaji vita wa daima kutekelezwa kati ya Wapalestina na utawala wa Israel ili kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo. Ameendelea kusema kuwa, utatuzi wa kisiasa ndiyo njia bora zaidi ya kutatua mzozo wa hivi sasa wa Palestina na kuyataka makundi yote ya Palestina kushirikiana kwa lengo la kurejesha amani na uthabiti wa kudumu katika ardhi zao.
Wakati huohuo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza imebainisha wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayotawala katika eneo hilo na kuzitaka nchi za dunia kutoa misaada ya kukarabatiwa Gaza na kutuma kwa haraka misaada ya kibinadamu katika ukanda huo ili kuwasaidia wahitaji wanaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu kufuatia mashambulio ya kinyama yaliyofanywa huko hivi karibuni na utawala wa Kizayuni. 377398