Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, kikao hicho kitafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Fedha ya Scotland na Baraza la Uwekezaji wa Kiislamu la nchi hiyo lenye makao yake katika mji wa Glasgow. Lengo la kufanyika kikao hicho limetajwa kuwa ni kuchunguza njia za kutoa huduma mbalimbali za uwekezaji kwa msingi wa sheria za Kiislamu.
Akizungumzia maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini humo katika uwanja wa uwekezaji wa Kiislamu, Sheikh Omar, Mkuu Baraza la Uwekezaji wa Kiislamu amesema kuwa kuna mashirika mengi ya Scotland ambayo yametoa maombi ya kunufaika na mbinu za uwekezaji wa Kiislamu katika shughuli zao za kiuchumi na kibiashara.
Amesema, hali ya hivi sasa inathibitisha kwamba watu wengi wanataka kushikamana na maadili pamoja na thamani za Kiislamu katika shughuli zao za kibiashara na kwamba uwekezaji wa Kiislamu ni dhihirisho halisi la maadili hayo. 379557