Ekmeledeen Ihsanoglu alitoa onyo hilo siku ya Jumatatu katika hotuba yake katika kikao cha viongozi wa nchi za Kiarabu huko Doha, Qatar. Amesisitiza kwamba, utawala wa Israel umekuwa ukiharibu na kubomoa kwa makusudi nyumba za Wapalestina wanaoishi Quds na hivyo kujaribu kufuta utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa mji huo mtakatifu, na kuzitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na hatua hizo haribifu za Wazayuni.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ihsanoglu ameashiria safari yake ya hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza uliokabiliwa na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni na ambao ungali upo chini ya mzingiro wa kidhulma wa utawala huo na kusema kuwa, athari za jinai za kivita na utumiaji utawala huo silaha zilizopigwa marufuku ni jambo lililo wazi na lisilokanushika kabisa.
Katibu Mkuu wa OIC amesisitiza kwamba kwa kuzingatia suala hilo, Waislamu wanapasa kufanya juhudi za kufuatilia na kuwafikisha wahusika wote wa jinai hizo katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
Ihsanoglu vilevile amezitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua za dharura za kukarabati uharibifu uliofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na pia kupunguza machungu ya waathirika wa jinai hizo kwa kuwafikishia misaada ya kibinadamu. 381656