IQNA

ISESCO kuhudhuria kikao cha Kamisheni ya Masuala ya Uchumi na Utamaduni ya OIC

11:18 - April 04, 2009
Habari ID: 1759891
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO litashiriki katika kikao cha pili cha Kamisheni ya Kiislamu ya Masuala ya Kiuchumi, Kiutamaduni na Kijamii ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kinachoanza leo hadi tarehe 6 Aprili katika mji wa Jiddah, Saudi Arabia.
Kikao hicho pia kinahudhuriwa na wawakilishi wa nchi 57 wanachama katika jumuiya ya OIC, jumuiya wanachama na taasisi za kitaalamu.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kigeni na Ushirikiano wa ISESCO atatoa ripoti kuhusu shughuli za shirika hilo tangu kikao cha kwanza hadi hivi sasa katika nyanja za elimu, sayansi na utamaduni.
Ripoti hiyo pia itagusia juhudi za ISESCO za kuiamarisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na jinsi ya kuzisaidia taasisi za kielimu na kiutamaduni katika nchi za Palestina, Iraq, Afghanistan na Somalia. 382103
captcha