IQNA

Kamati ya kuchunguza jinai za Wazayuni Gaza yaundwa

8:57 - April 06, 2009
Habari ID: 1760781
Kamati ya kimataifa ya kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza inayoongozwa na Richard Goldstone, mwanasheria mashuhuri wa Kiyahudi raia wa Afrika Kusini, imebuniwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
Mwanasheria huyo ambaye ni mkaguzi wa zamani wa vita vya Yugoslavia, amesema kuhusiana na suala hilo kwamba amepewa jukumu la kuchunguza jinai zote zilizotekelezwa na utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza. Amesema kuwa ameshangazwa kuteuliwa kwake kuongoza kamati hiyo kwa kuzingatia kuwa yeye mwenyewe ni Myahudi lakini akaongeza kuwa, ana imani kuwa ataweza kutekeleza jukumu hilo muhimu kitaalamu kwa kushirikiana na wanakamati wenzake, na kuwasilisha matokeo ya wazi na ya kuaminika kuhusianana suala hilo.
Richard Goldstone amesema, ili kuwasilisha ripoti kamilifu kuhusiana na suala hilo kamati hiyo inahitajia muda wa kutosha. Ameelezea matumaini yake kwamba kamati hiyo itafanikiwa kutatua baadhi ya masuala muhimu ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel na hivyo kuleta amani na utulivu wa kudumu katika radhi hizo.
Katika hujuma ya kinyama iliyotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha siku 22, Wapalestina wasio na hatia 350 wakiwemo watoto na wanawake walipoteza maisha yao na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa.
Hasara ya zaidi ya dola bilioni tatu pia ilisababishwa na utawala huo dhidi ya makazi na miundombinu ya ukanda huo.
383063
captcha