IQNA

Mkutano wa Jumuiya ya Ulimwenu wa Kiislamu kufanyika Barani Afrika

15:48 - April 06, 2009
Habari ID: 1761104
Mkutano wa mafunzo na ulinganiaji wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Ulimwengu wa Kislamu (Muslm World League) unatazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu baani Afrika.
Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni kueneza utamaduni wa Kiislamu katika nchi za Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya Waislamu wa bara hilo na taasisi za Kiislamu duniani.
Jumuiya ya Muslim World League imetangaza kwamba Katibu Mkuu wake Abdulmuhsin al Turki atazitembelea nchi za Nigeria, Benin, Sierra Leon Chad na Djibout kueleza mipango ya Kiislamu ya jumuiya hiyo na kuchunguza hali ya Waislamu wa maeneo hayo. Al Turki atakutana na kuzungumza na maimamu wa misikiti, viongozi wa jumuiya mbalimbali na wahubiri wa Kiislamu. 383301

captcha