Mashindano hayo ya Qur'ani ya kitaifa yanafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa kipindi cha miezi miwili na washindi wa kwanza katika kila mkoa watashiriki katika fainali ya mashindano ya Qur'ani mjini Dar es Salaam ambayo itaainisha wawakilishi wawili wa nchi hiyo katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya kimataifa mjini Tehran.
Fainali ya mashindano hayo itahudhuriwa na mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Salma Kikwete.
Bi Salma Kikwete pia atasoma Qur'ani katika fainali ya mashindano hayo ambayo itarushwa hewani na redio ya taifa ya Tanzania. 383663