IQNA

ISESCO kuchunguza harakati za utawala wa Kizayuni katika msikiti wa al Aqsa

0:09 - April 12, 2009
Habari ID: 1763331
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO litafanya kikao maalumu tarehe 15 Aprili katika mji mkuu wa Jordan Amman kuchunguza harakati za utawala ghasibu wa Israel za kuchimba mashimo chini ya msikiti wa al Aqsa.
Mkutano huo wa siku mbili utakuwa wa pili wa ISESCO unaojadili kadhia ya mashimo yanayochimbwa na utawala wa Kizayuni wa Israel chini ya msikiti mtukufu wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Mkutano huo utahudhuriwa na wataalamu wa athari za kale wa ISESCO, Jordan na Palestina.
Wataalamu hao watajadili na kuchunguza jinai za hivi karibuni za Israel katika eneo la Quds na msikiti wa al Aqsa na taathira za mashimo yanayochimbwa na utawala huo haramu dhidi ya turathi za Kiislamu za maeneo hayo.
Vilevile ISESCO itawasilisha ripoti kuhusu njama za Wazayuni za kubadilisha utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa Palestina. 385692
captcha