Hayo yamesemwa na Amir wa Makka Khalid al Faisal ambaye pia ameashiria nafasi muhimu ya mji huo kati ya Waislamu kote duniani. Al Faisal amesema katika kikao cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa mjini Jiddah wanaochunguza miradi ya mji wa Makka kwamba zinafanyika jitihada za kutatua baadhi ya matatizo ya mji huo.
Amesisitiza kuwa kupitia miradi hiyo, mji wa Makka utabadilishwa na kuwa moja ya miji ya kisasa na maridadi zaidi duniani kulingana na hadhi yake ya kihistoria na Kiislamu na kuwa fahari ya Waislamu wote.
Amesema kuwa kikao hicho cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa ni fursa nzuri ya kushirikiana katika jitihada za kustawisha ujenzi wa mji wa Makka na kusahilisha kuingia na kuondoka mahujaji katika mji huo mtakatifu. 386483