Akizungumzia suala hilo, Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Hassan Muradi, Mkuu wa Baraza la Uratibu wa Uhubiri wa Kiislamu katika mkoa wa Khuzestan nchini Iran amesema kuwa dunia ya leo ni dunia ya maendeleo na ustawi inayoshuhudia wimbi kubwa la mfumuko wa elimu na habari.
Sheikh Hassan Muradi amesema kuhusiana na jambo hilo kwamba Waislamu wana nguzo kadhaa muhimu wanazotegemea kuhusiana na suala la elimu ikiwemo Qur'ani Tukufu, Mtume Muhamad (saw) na Imam Ali (as) ambaye amesifiwa na Mtume kuwa ni lango la kuingilia katika jiji la elimu ambalo ni Mtume mwenyewe.
Amesema kati ya vitabu 104 vya mbinguni vilivyoko duniani vyote vimepotoshwa na mikono ya wanadamu isipokuwa Qur'ani pekee ambayo Mwenyezi Mungu amesema kuwa ndiye anayeilinda isipatwe na upotofu. 389098