IQNA

Kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu hakuma maana ya kuzifuta

16:45 - April 21, 2009
Habari ID: 1768104
Maulamaa na wanazuoni wa Kiislamu wanapaswa kuratibu masuala yanayowakutanisha pamoja Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni na kuyafanya muhimili wa umoja na mshikamano wa wafuasi wote wa dini hiyo.
Wanazuoni hao wanapaswa kuelewa kwamba kukurubisha pamoja madhehebu hizo mbili hakuna maana ya kuangamiza moja kwa maslahi ya jingine.
Hayo yamesemwa na Ayatullah Ja'far Subhani katika mazungumzo yake na wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiisalmu. Ayatullah Subhani amesema kuwa maulamaa wanapaswa kukusanya masuala yanayowakutanisha pamoja wafuasi wa madhehebu za Shia na Suni na kufanya mijadala ya kielimu kuhusu masuala yanayozusha hitilafu kati ya pande hizo.
Amesisitiza kuwa huko nyuma maulamaa wa Shia na Suni walikuwa wakikutana na kujadili masuala mbalimbali ya kielimu lakini inasikitisha kwamba katika kipindi cha sasa kumejitokeza hitilafu ambazo zimezua mtengano kati ya pande hizo mbili. Ametoa mfano wa mazungumzo na mawasiliano yaliyofanywa katika miaka ya nyuma kati ya Ayatullah Burujerdi na Sheikh wa wakati huo wa al Azhar Mahmoud Shaltut na akasisitiza juu ya kufuatiliwa suala la kukurubisha pamoja wafusi wa mashehebu za Shia za Suni. 391536
captcha