IQNA

Kuanza kusajiliwa majina ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani ya Masjidul Haram

8:20 - April 25, 2009
Habari ID: 1769092
Majina ya washiriki wa duru ya nane ya washiriki wa mashindano ya kimataifa ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika mwaka huu wa 1430 Hijiria yalianza kusajiliwa siku ya Alkhamisi katika Msikiti Mtukufu wa Makka au kwa jina jingine Masjidul Haram.
Kwa mujibu wa gazeti la Madina la nchini Saudi Arabia, Swalah bin Ali az-Zami' mkuu wa duru hii ya mashindano amesisitiza kwamba washiriki hawatakabiliwa na vikwazo wala masharti yoyote ya umri, jinsia wala maeneo ya kijografia. Amesema kwa mara ya kwanza, mashindano hayo yalifanyika mjini Makka mwaka 1422 Hijiria ambapo yaliwashirikisha washindani 10 kwa kipindi cha siku 60, ambapo raia wa Umoja wa Falme za Kiarabu ndiye aliyeibuka msindi kwa kufanikiwa kuhifadhi Qur'ani katika kipindi cha siku 27. Amesema kuhifadhiwa juzuu moja na nusu ya Qur'ani kila siku na kuandaliwa kwa vikao vya kusoma Qur'ani kwa mbinu ya tajweedi ni miongoni mwa ratiba thabiti za mashindano hayo.
Swalah bin Ali az-Zami' ameongeza kuwa, hadi sasa wavulana na wasichana 1500 wamefanikiwa kuhifadhi Qur'an na pia kuhitimu mafunzo ya kufunza kitabu hicho kitakatifu katika kipindi cha duru hii ya nane ya mashindano. Amesema maelezo zaidi kuhusiana na mashindano hayo yanaweza kupatikana kupitia mtandao kwa anwani ifuatayo: www.qurani.co. 393656

captcha