IQNA

Dubai, mwenyeji wa mashindano ya 'Kwa Qur'ani Tutakuwa Hai'

8:39 - April 25, 2009
Habari ID: 1769097
Taasisi ya Masuala ya Kiislamu na ya Kheri ya Dubai imeandaa mashindano chini ya anwani ya 'Kwa Qur'ani Tutakuwa Hai' katika mikoa yote ya Umoja wa Falme za Kiarabu, mashindano ambayo yalianza siku ya Alkhamisi na kuhudhuriwa na washiriki 142.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Imarati, Aisha al-Kash mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo amesema kuwa lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuimarisha na kueneza dini miongoni mwa tabaka la watoto na vijana na kuwashajiisha wahifadhi Qur'ani Tukufu. Amesema kugunduliwa kwa vipaji vya Qur'ani katika nyanja za kuhifadhi, kusoma, tartil, tafsir na pia kutafuta njia za kuimarisha ushirikiano na vituo vya mafunzo ya Qur'ani ni malengo mengine ya kufanyika mashindano hayo.
Samira la-Fuheimi msimamizi mwingine wa mashindano hayo amesema, mashindano hayo ambayo yatendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili yatafanyika katika sehemu tatu za shule za chekechea; katika kuhifadhi sura za Adiyaat hadi an-Nas, darasa la kwanza na pili; kuhifadhi sura za al-Ghashiya hadi az-Zilzal na darasa la tatu; kuhifadhi sura za an-Nabaa hadi al-A'la. 393633
captcha