Harakati ya Kimataifa ya Kutetea Haki za Watoto, imetoa taarifa ikielezea wasiwasi wake mkubwa na wakati huohuo kukosoa vikali hatua ya utawala haramu wa Israel za kushinikiza, kuzingira na hata kuwakamata watoto wadogo huko katika Ukanda wa Gaza na Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.