IQNA

Wafaransa waandamana leo dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

10:31 - May 02, 2009
Habari ID: 1772508
Waislamu wa Ufaransa watafanya maandamano hii leo mjini Paris kupinga hujuma inayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msikiti wa al Aqsa na njama za Israel za kulifanya eneo la Quds Tukufu kuwa la Kiyahudi.
Mwandishi wa IQNA nchini Ufaransa amesema kuwa Waislamu nchini humo wataandamana katika medani ya Enfert Rochereau wakipinga harakati za kibaguzi za utawala ghasibu wa Israel. Mandamano hayo yanafanyika kufuatia kushadidi kwa harakati za Israel za kuharibu msikiti wa al Aqsa na ujenzi wa mahekalu mia moja ya Kiyahudi kandokando ya msikiti huo.
Baadhi ya makundi na jumuiya za Kiyahudi katika siku za hivi karibu zilitoa taarifa zikitaka kufukuzwa Wapalestina katika eneo la Quds na kufanyika shughuli za ibada za Mayahudi ndani ya msikiti wa al Aqsa. Suala hilo limekabiliwa na upinzani mkubwa wa jumuiya na taasisi za Kiislamu.
Utawala wa Kizayuni umewapiga marufuku Wapalestina wenye umri wa chini ya miaka hamsini kuingia katika msikiti wa al Aqsa. 397650

captcha