IQNA

Kikao cha Mauritania na Senegal, kuleta mabadiliko makubwa katika umoja wa OIC

8:51 - May 04, 2009
Habari ID: 1773398
Akifungua kikao cha kwanza cha Kiislamu cha nchi za Senagal na Mauritania mjini Dakar, Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amesema kuwa kuandaliwa kikao hicho kutaleta mabadiliko makubwa katika Jumuiya ya Nchi Kiislamu OIC.
Rais Abdoulaye Wade ambaye ni Mwenyekiti wa hivi sasa wa jumuiya hiyo amesema kuwa, kikao hicho cha Senegal ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa wanazuoni wa Senegal na Mauritania, ni fursa nzuri kwa wanazuoni hao kuzungumza na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali, jambo ambalo amesema bila shaka litaleta mabadiliko makubwa katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu.398660
captcha