IQNA

Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Ustawi:

Mfumo wa zamani, changamoto kubwa kwa huduma za benki za Kiislamu

8:18 - May 04, 2009
Habari ID: 1773452
Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Ustawi amesema kuwa nchi nyingi zinazotoa huduma za kifedha za Kiislamu zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria za taasisi za kifedha za zamani, suala ambalo ndilo changamoto kubwa kwa maendeleo ya huduma za kifedha za Kiislamu.
Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Ustawi Ahmad Muhammad Ali amesema hayo katika mkutano wa kimataifa wa wanasheria wa sekta ya huduma za kifedha za Kiislamu mjini Jiddah Saudi Arabia na akaongeza kuwa kwa sasa udhaifu wa muundo wa kisheria wa sekta ya huduma za kifedha za Kiislamu ndio changamoto kubwa ya sekta hiyo na kwamba inasikitisha kwamba taasisi za kifedha za Kiislamu katika nchi mbalimbali hazijaafikiana juu ya namna ya kuondoa hitilafu zao.
Muhammad Ali ameashiria pia upungufu wa wataalamu wa sheria katika sekta ya fedha ya Kiislamu na akasema mgogoro mkubwa wa kifedha uliozikumba benki na taasisi za fedha duniani umekuwa na taathira ndogo kwa sekta ya huduma ya fedha ya Kiislamu.
Benki ya Kiislamu ya Ustawi ambayo iliasisiwa mwaka 1975 ni taasisi ya kifedha ya kimataifa inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. 398622
captcha