IQNA

Kusambazwa filamu ya "Kuondoa Shaka, Muhtasari Kuhusu Uislamu" huko North Carolina

17:34 - May 05, 2009
Habari ID: 1774118
Nakala elfu 20 za filamu ya "Kuondoa Shaka, Muhtasari Kuhusu Uislamu" zimeanza kusambazwa katika jimbo la North Carolina nchini Marekani.
Gazeti la The News & Observer limeripoti kuwa Jumuiya ya Waislamu wa Marekani imechukua hatua ya kusambaza filamu hiyo kujibu uchapishaji wa matangazo yanayochafua jina la Uislamu katika vyombo vya habari vya Marekani yanayobeba anwani: Kufurutu Mipaka, Vita vya Uislamu wenye Misimamo Mikali Dhidi ya Magharibi".
Filamu ya Kuondoa Shaka, Muhtasari Kuhusu Uislamu ambayo imetayarishwa na kampuni moja ya Misri, inalenga kuarifisha sura halisi ya Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu na kuondoa shaka na sura mbaya iliyoenezwa kati ya watu kuhusu dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Katika filamu hiyo pia kumebainishwa mitazamo ya wanafalsafa mashuhuri kama Aristotle, Rene Descartes na Auguste Komte kuhusu Mwenyezi Mungu na mitazamo ya watu mashuhuri kama Gandi na Goethe kuhusu Mtume Muhammad (saw). 398968

captcha