IQNA

Msomi atoa wito wa kuundwa kwa Umoja wa Kiislamu kupinga ubeberu wa Magharibi

16:52 - September 22, 2025
Habari ID: 3481270
IQNA – Mwanasiasa na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Iran ametoa wito kwa nchi zenye Waislamu wengi kuunda umoja wa kisiasa na kiuchumi ili kuimarisha msimamo wao wa pamoja dhidi ya miungano ya mataifa ya Magharibi kama vile NATO na Umoja wa Ulaya.

Hujjatul-Islam Seyed Sajjad Izdehi, mhadhiri mshiriki wa siasa katika Taasisi ya Utafiti wa Utamaduni na Fikra ya Kiislamu, alisema kuwa mataifa ya Kiislamu yaliyo katika hali ya kutawanyika lazima yatafute njia za kushirikiana na kuratibu juhudi zao, hasa pale ambapo hayawezi kujisimamia peke yao dhidi ya vitisho vya nje.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika Jumapili, alisema: “Nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa imara na zenye nguvu ili kukabiliana na maadui. Ikiwa mataifa madogo hayawezi kufanya hivyo kibinafsi, basi ni lazima yaungane.”

Izdehi alitaja Umoja wa Ulaya na NATO kama mifano ya jinsi mataifa yenye tawala tofauti na hata migongano ya ndani yanavyoweza kuendeleza mikakati ya pamoja katika masuala ya ulinzi, usalama, na sera za kiuchumi.

“Barani Ulaya kuna sauti nyingi,” alisema. “Hata kati ya Marekani, Ulaya na Israel kuna mitazamo tofauti, lakini linapokuja suala la usalama na ulinzi, wanachukua msimamo wa pamoja na kuunda nguvu ya pamoja.”

Alieleza kuwa mataifa ya Kiislamu yanaweza kufuata njia kama hiyo: “Umoja wa pamoja kati ya nchi za Kiislamu, sambamba na mikataba, mfuko wa pamoja, sarafu ya pamoja, na soko la pamoja, lazima uanzishwe, kwani hili litazalisha nguvu ya pamoja.”

Izdehi aliongeza kuwa aina mpya za ushirikiano kama vile Shirika la Ushirikiano la Shanghai zinaweza kusaidia kuimarisha mshikamano wa Kiislamu, kwa lengo la kupunguza ushawishi wa Magharibi na NATO katika masuala ya kimataifa.

3494704

Habari zinazohusiana
captcha