Kwa mujibu wa tovuti ya habari radioalgerie.dz, tukio hili la Qur’ani linafanyika chini ya udhamini wa Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, na ndani ya muktadha wa maadhimisho ya Maulidi ya Mtume Muhammad (SAW).
Shughuli na vipindi vya Wiki ya Qur’ani ya mwaka huu vimepangwa chini ya kaulimbiu: “Kutoka kwenye mimbari za misikiti yetu, mshikamano wa taifa letu hujengeka.”
Vipindi hivyo vinajumuisha mashindano ya kitaifa ya Qur’ani katika makundi sita tofauti.
Hatua ya mkoa ya mashindano hayo, isipokuwa ya usomaji wa Qur’ani, ilifanyika kuanzia Julai 1 hadi Agosti 7, 2025.
Wiki ya Qur’ani pia itajumuisha mkusanyiko wa kitaifa wa kielimu unaoitwa: “Ushikamano wa Kijamii na Mshikamano wa Kitaifa kwa Mujibu wa Maadili ya Qur’ani.”
Mkutano huo utahudhuriwa na mashaykh wa Zawiyyah (vyuo vya jadi vya elimu ya Qur’ani), wanazuoni, na maimamu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika ya Kaskazini, ambapo Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia tisini na tisa ya wakazi wake.
3494568