IQNA

Nchi 70 zashiriki Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani ya Libya mjini Benghazi

14:57 - September 21, 2025
Habari ID: 3481261
IQNA – Mji wa Benghazi ulioko kaskazini mashariki mwa Libya ni mwenyeji wa toleo la 13 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya nchi hiyo.

Mashindano hayo yanayojulikana kama, Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Libya, yameanza rasmi mapema wiki hii, na yanahesabiwa kama  tukio mashuhuri la kidini na kitamaduni linalowakutanisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 70 duniani.

Ushiriki huu wa kiwango cha juu unaonesha umuhimu rasmi ambao serikali ya Libya inaupa mashindano haya ya kimataifa ya Qur’ani, sambamba na kujitolea kwake katika kuunga mkono na kudhamini shughuli za kidini zinazokuza utambulisho wa Kiislamu na kiroho wa jamii.

Tuzo hii ya Kimataifa ya Qur’ani ya Libya inachukuliwa kuwa miongoni mwa mashindano muhimu ya Qur’ani, ambapo kila toleo huvutia kundi la wasomi wa Qur’ani kutoka mabara mbalimbali kushindana katika mazingira ya imani na unyenyekevu, yakiongozwa na maadili ya udugu, mapenzi, na amani kama inavyofundishwa na Qur’ani Tukufu.

70 Countries Attending Libya Int’l Quran Award in Benghazi

Toleo la sasa linatarajiwa kushuhudia ushindani mkali miongoni mwa washiriki.

Libya ni nchi ya Kiislamu iliyoko Afrika Kaskazini, yenye zaidi ya wahifadhi milioni moja wa Qur’ani Tukufu. Hata hivyo, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochochewa na na NATO mwaka 2011 ambavyo vilisababisha kuondolewa na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi, nchi hiyo imekumbwa na hali ya machafuko. Katika miaka ya karibuni, Libya imegawanyika kati ya serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoko Tripoli na utawala wa mashariki unaojitegemea.

3494679

captcha