IQNA

Baraza la Wahindu latuhumiwa kwa Chuki Dhidi ya Uislamu nchini Australia

18:38 - September 23, 2025
Habari ID: 3481273
IQNA – Tume ya Haki za Binadamu ya Australia imeanzisha uchunguzi kufuatia malalamiko dhidi ya Baraza la Wahindu la Australia, likiwemo Rais wake Sai Paravastu na Mkuu wa Idara ya Habari Neelima Paravastu, wakidaiwa kujihusisha mara kwa mara na matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu kuanzia Mei 2024 hadi Julai 2025.

Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa na muungano wa Muungano wa Kukabiliana na Chuki Dhidi ya Uislamu (Alliance Against Islamophobia), maudhui ya mitandao ya kijamii na kauli za hadharani zililenga Waislamu wa India, Bangladesh, na jamii ya Rohingya, kwa kushiriki maudhui kutoka kwa watu wa mrengo mkali wa kulia na kuwasilisha Waislamu kama wahalifu wa asili, hatari, au tishio kwa jamii.

Malalamiko hayo yanasema kuwa baadhi ya machapisho yalitoa taswira kwamba Waislamu ni “wahalifu, wenye jeuri, au waovu kwa asili,” “huwalenga watoto, wazee na wanyonge,” na “kwa ujumla ni tishio kubwa kwa jamii,” kwa mujibu wa gazeti la The Guardian.

Muungano huo unataka Baraza hilo litowe msamaha wa hadharani, kuondoa machapisho hayo, kutoa ahadi za kisheria za kutoendeleza matusi au chuki, na fidia kwa madhara ya kiakili yaliyosababishwa.

Tangu kuanza kwa vita kati ya utawala wa Israeli na Hamas huko Gaza mnamo Oktoba 2024, ripoti zinaonyesha ongezeko kubwa la matukio ya chuki dhidi ya Waislamu nchini Australia. Matukio ya moja kwa moja yameongezeka kwa takriban asilimia 150, huku yale ya mtandaoni yakipanda kwa takriban asilimia 250.

Utafiti wa mwaka 2024 ulibaini kuwa kati ya Januari 2023 hadi Novemba 2024, zaidi ya matukio 600 ya chuki dhidi ya Uislamu yalithibitishwa, mtandaoni na ana kwa ana, huku wanawake wakiathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.

3494713

captcha