Mkutano huo ulifanyika jioni ya Jumatatu pembeni mwa Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu.
Katika tamko lao la mwisho, washiriki walieleza:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Imepita takriban miaka miwili tangu utawala wa Kizayuni uanze mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya sehemu za ardhi za Kiislamu, na kwa ujasiri wa dhulma na tabia ya kinyama, umeendelea kuongeza kina na wigo wa jinai zake kila uchao.
Mwaka jana, tulipokutana kama wanawake kutoka nchi za Kiislamu, mashambulizi ya Kizayuni yalikuwa hayajavuka sana mipaka ya Gaza. Lakini kwa kuona ukimya wa baadhi ya sehemu muhimu za ulimwengu wa Kiislamu na kuona watu wa Gaza wakiachwa peke yao, Wazayuni wamepata ujasiri wa kupanua mashambulizi yao hadi maeneo mengine ya ardhi za Kiislamu kama vile Ukingo wa Magharibi, Lebanon, Sanaa nchini Yemen, na hata Tehran na miji mingine ya Iran ya Kiislamu.
Naam, wanashambulia mataifa na majeshi ambayo yameamua kusimama upande wa haki na kuunga mkono wanyonge, wakifuata mafundisho ya ndugu na khalifa wa Mtume Muhammad (SAW),Imam Ali (A.S.),aliyesema: “Kuwa adui wa dhalimu na msaidizi wa mnyonge.”
Tunapaswa pia kutambua msimamo wa wanawake wa Iran katika vita vya siku 12 vilivyolazimishwa na Israel mwezi Juni, ambao walionesha mfano wa kujitolea na subira katika kukabiliana na maafa na hasara zilizosababishwa na uvamizi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni.
Tamko la Mwisho la Wanawake Waislamu:
Katika kukosekana kwa msimamo madhubuti wa serikali za Kiislamu katika kuwatetea watu wa Gaza, Lebanon na Yemen, sisi wanawake kutoka nchi za Kiislamu tunatangaza yafuatayo:
1. Ukimya mbele ya madhalimu hautaleta usalama, bali utawafanya kuwa watumwa wa maslahi yao haramu.
2. Hatima ya watu wa Gaza haijitengi na hatima ya mataifa mengine ya Kiislamu katika eneo hili. Ukimya na kutochukua hatua za kivitendo kutasababisha yaliyowapata Wapalestina kuwakumba Waislamu wengine pia.
3. Upatikanaji wa maji salama na chakula kwa watu wa Gaza, hususan wanawake na watoto, unapaswa kuwa matakwa ya msingi ya mataifa ya Kiislamu na kipaumbele cha tawala zote za Kiislamu.
4. Kususiwa kwa kina kwa utawala wa Kizayuni lazima kuwe sehemu ya ajenda ya tawala za Kiislamu. Shughuli zote za kiuchumi, kibiashara, na mahusiano ya aina yoyote zinapaswa kupigwa marufuku kabisa.
5. Tunatoa shukrani na pongezi kwa wanachama wa mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu, hususan wanaharakati wa kiraia, waandishi wa habari, na watetezi wa haki za wanawake duniani kote, waliowajibika kusimama na watu wa Gaza na kwa kuandaa maandamano maelfu, walifikisha kilio cha Wapalestina kwa dunia nzima.
3494540