IQNA

Mbunge wa Bunge la Marekani asema anajivunia Uislamu wake

15:40 - September 21, 2025
Habari ID: 3481264
IQNA – Mjumbe wa chama cha Democratic katika Bunge la Marekani, Bi Ilhan Omar, amesisitiza utambulisho wake wa Kiislamu, akisema anajivunia kuwa Mwislamu.

Katika kujibu mashambulizi ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyemkosoa kwa asili yake ya Kisomali na maisha yake binafsi, Bi Omar aliandika kwenye mtandao wa X kwamba anajivunia mizizi yake ya Kiislamu na Kisomali, pamoja na uraia wake wa Marekani.

Katika chapisho lake mnamo tarehe 20 Septemba 2025, masaa machache baada ya ujumbe wa Trump kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social kumtusi kwa kummtaja kama “SCUM” yaani takataka, Omar aliandika: “Ninajivunia kuzaliwa Mwislamu. Ninajivunia kuzaliwa Somalia. Ninajivunia kuwa raia wa Marekani. Hakuna yeyote kati yenu anayeweza kubadilisha hilo, haijalishi mnatwiti kwa hasira kiasi gani. Kunyweni maji na mguse majani.”

Chapisho hilo lilipata zaidi ya likes 44,000, reposts 3,800, na takriban watazamaji milioni moja ndani ya masaa machache, na lilizua uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa washirika wake wa kisiasa, huku wakosoaji wa kihafidhina wakilalamika.

Tukio hili lilifuatia matamshi ya Trump mnamo Septemba 19, aliyoiita Somalia kuwa nchi “iliyojaa umasikini, ugaidi na ufisadi,” akitilia shaka haki ya Omar kushiriki katika sera za Marekani.

Soma Zaidi:

 Mwanamke wa Kwanza Mwislamu Kula Kiapo kwa Qur’ani Bungeni Marekani

Bi Ilhan Omar, mwakilishi wa jimbo la Minnesota na mmoja wa wanawake wa kwanza Waislamu kuingia Bunge la Marekani, amekuwa akishambuliwa mara kwa mara na Trump, ikiwemo wito wa mwaka 2019 wa kumfukuza nchini. Majibu yake yamekuwa yakisisitiza ustahimilivu mbele ya ubaguzi wa rangi.

Tukio hili linaonesha mgawanyiko wa kisiasa unaoendelea nchini Marekani, huku chapisho la Trump likiongeza nguvu kwa jaribio lililoshindikana la chama cha Republican kumkemea Omar wiki iliyopita kufuatia kauli zake kuhusu kuuawa kwa mwanaharakati mwenye misimamo mikali aliyekuwa mfuasi  sugu wa Trump.

 

 

Habari zinazohusiana
captcha