IQNA

Uislamu ndio chimbuko la aghlabu ya sayansi

9:45 - May 06, 2009
Habari ID: 1774516
Mwanazuoni mmoja wa Iran amesema chimbuko la aghlabu ya sayansi muhimu duniani ni Uislamu na wasomi wa Kiislamu.
Ayatollah Sayyid Izzuddin Zanjani ambaye ni kati ya Marjaa Taqlid katika mji mtakatifu wa Mashhad ameongeza kuwa mwanadamu anapaswa kufuatilia kwa kina suala la kujifunza sayansi mbalimbali.
Katika mkutano wake na walinganiaji wa Kiislamu katika mkoa wa Khurasan Razavi, Ayatullah Zanjani ametoa shukrani kwa wanazuoni wakubwa wa Kishia waliotangualia kama vile Khaja Nasiruddin Tusi, Farabi na Sheikh Bahai na kusema wanazuoni hao walitabahari katika sayansi na elimu mbalimbali kama vile hisabati. Amesema chimbuko la aghalabu ya sayansi ni wasomi wa Kiislamu.
Ameashiria mwanazuoni bingwa wa Kishia, Marhum Ayatullah Haj Sheikh Muhammad Hussein Isfahani na kumtaja kuwa alikuwa msomi bingwa katika uga wa Fiqhi na Usoli.
Kuhusu Khaja Nasiruddin Tusi, Ayatullah Zanjani amesema, nadhari za msomi huyo bingwa zinategemewa sana na watafiti wa bara ulaya ambao wanakiri kwamba alikuwa msomi wa kipekee.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Zanjani amekumbusha kuhusu dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiya na amesisitiza juu ya umuhimu wa kutiliwa maanani kitabu hicho cha dua. 399846
captcha