IQNA

Mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani yafanyika nchini Saudi Arabia

9:38 - May 06, 2009
Habari ID: 1774570
Mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Amir Salman bin Abdul Aziz yalianza siku ya Jumatatu huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia SPA, Ibrahim bin Suleiman al-Huweimal, mwanachama wa kamati ya marefa wa mashindano hayo amesema kuwa katika hatua ya kwanza ya mashindano hayo, wanaume 17 na wanawake 11 walishindana katika usomaji wa kitabu hicho kitakatifu. Huku akiashiria kwamba kwa mara kwanza kabisa tafsiri ya maneno ya Qur'ani imejumuishwa katika mashindano hayo, al-Huweiman amesema kuwa kamati iliyoandaa mashindano hayo imewatengea washindi wa kwanza hadi tatu wa hatua zote tano za mashindano hayo zawadi ya pesa taslimu zipatazo riali 600,000.
Vilevile katika siku ya kwanza ya mashindano hayo wakuu wa vituo vya uhifadhi na usomaji Qur'ani vya nchini Saudi Arabia walishiriki katika mashindano hayo na kutaka yaakisiwe vyema katika vyombo vya habari.
Mashindano hayo yaliyoanza Jumatatu yataendelea katika mji wa Riyadh kwa muda wa siku 10. Mashindano hayo yanafanyika kwa utaratibu ufuatao: Kuhifadhi Qur'ani nzima, kusoma, tajweed na tafsiri ya maneneo ya Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani nzima, kusoma Qur'ani nzima, kusoma na tajweed, kuhifadhi juzuu 20, kusoma na tajweed, kuhifadhi juzuu 10, kusoma na tajweed na hatimaye kuhifadhi juzuu 5, kusoma na tajweed. 400124
captcha