Kikao cha kieneo cha 'Mwanamke katika Mtazamo wa Qur'ani' kimefanyika kwa juhudi za pamoja za Wizara ya Masuala ya Wanawake ya Afghanistan na Taasisi ya Shahid Balkhi na kwa ushirikiano wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.
Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza siku ya Jumanne kinafanyika kwa mara ya kwanza katika fremu ya kieneo.
Fatuma Zahra, mbunge katika Majlisi ya Ushauri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Swadiqa Hijazi, Mkuu wa Masuala ya Wanawake na Familia katika Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu, Zahra Rasti, Mkuu wa Eneo la Kwanza la Masomo ya Wanawake mjini Tehran ambaye anamwakilishi Tayyib Zadeh, Mshauri wa Rais wa Iran kuhusiana na Masuala ya Wanawake na Familia na wahadhiri kadhaa wa vyuo vikuu vya kidini na visivyo vya kidini wanashiriki katika kikao hicho ambacho lengo lake kuu ni kuchunguza mitazamo ya Kiislamu na Qur'ani kuhusiana na wanawake na familia.
Ujumbe wa wanawake wa Iran wanaoshiriki katika kikao hicho pia umeonana na kuzungumza na makamu wa pili wa rais wa Afghanistan. 401011