IQNA

Kuanza tamasha ya filamu fupi za Mapambano na Gaza

11:40 - May 07, 2009
Habari ID: 1775122
Tamasha ya kwanza ya filamu fupi ya Mapambano na Gaza inayofanyika chini ya anwani: 'Ardhi ya Zetuni' na inayofanyika sambamba na nyingine kama hiyo mjini Tehran Iran ilianza siku ya Jumanne kwa sherehe maalumu katika ukumbi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon.
Maafisa wa Hizbullah ya Lebanon, wanadiplomasia wa Iran, wasanii wa nchi mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu na wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za kiutamaduni na kisanii za nchi hizo wanashiriki katika tamasha hiyo. Waandaaji wa tamasha hiyo wanasema kuwa, mbali na Lebanon na Iran, matamasha kama hayo yanafanyika pia katika nchi za Qatar na Sudan.
Ali Dhwahir mmoja wa wakuu wa uenezaji habari wa Hizbullah amesema kuwa, tamasha hiyo ya filamu fupi imefanyika kutokana na hamu kubwa ya nchi mbalimbali na hasa za Ulaya kuvutiwa na filamu fupi, na kuelezea imani yake kwamba tamasha hiyo ya kiutamaduni bila shaka itawavutia vijana wengi wasanii katika nchi za Kiarabu na Kiislamu na vilevile za Ulaya. Filamu fupi na mashuhuri ya Tantura ambayo ilishinda tuzo la filamu ya Algeria mwaka uliopita na ambayo inazungumzia kutekwa na kuuawa kwa wakazi wa kijiji cha Tantura na maghasibu wa Kizayuni, imeonyeshwa katika ufunguzi wa tamasha hiyo. 400973
captcha