Akizungumza na Abu Dharr Ibrahim Turkman, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko mjini Moscow Russia, Fokin amesema kuwa mara hii ni ustaarabu wa Iran ndio utakaoarifishwa katika kikao hicho ambacho kimepangwa kufanyika mwezi Oktoba, kama ilivyofanyika kuhusiana na kuarifishwa utamaduni wa Uchina mwaka uliopita. Amesema kuwa kamati ya kikao hicho cha mazungumzo ya staarabu inatazamia kurekodi filamu ya kweli ya dakika 52 kuhusiana na Iran ambayo imepangwa kuonyeshwa katika kanali ya kwanza ya televisheni ya Russia. Kwa upande wake Ibrahimi, amesema kuwa fikra ya kufanyika mazungumzo ya staarabu mbalimbali kati ya jamii tofauti ambayo ilipendekezwa na Jamhuri ya Kiislamu na kutekelezwa na Umoja wa Mataifa imewavutia wengi duniani kutokana na athari zake za kuimarisha amani na uthabiti ulimwenguni. 402190