IQNA

Kitabu cha Kiongozi Maudhamu chauzwa kwa wingi zaidi kati ya vitabu vya Ofisi ya Usambazaji Utamaduni wa Kiislamu

9:40 - May 10, 2009
Habari ID: 1776061
Mkurugenzi Mwandamizi wa Ofisi ya Usambazaji Utamaduni wa Kiislamu amesema kuwa kitabu cha Matlae Eshq cha Ayatullahil Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ndicho kitabu kilichouzwa kwa wingi zaidi kati ya vitabu vinavyouzwa na ofisi hiyo.
Kitabu hicho kinazungumzia nasaha za kidini na kiirfani za Kiongozi Muadhamu kwa vijana waliofunga ndoa. Akizungumza na shirika la habari la IQNA, Hussein Mahdiyan, amesema kuwa nasaha zilizomo katika kitabu hicho zimekusanywa na kuandikwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Ali Akbari. Ameashiria kuchapishwa upya kwa vitabu vya Sayyid Jaafar Shahidi, na kusema kuwa, vitabu vyake vingine vimechapishwa kwa mara ya 40 na kwamba baadhi ya matoleo ya vitabu hivyo yamechapishwa katika kopi laki tano. Ameendelea kusema, baadhi ya vitabu vinavyoonyeshwa katika kibanda cha ofisi hiyo ya uchapishaji na usambazaji vitabu havipatikani katika vibanda vingine vyote katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayoendelea hivi sasa mjini Tehran. Ofisi hiyo ya usambazaji utamaduni wa Kiislamu imekuwa ikiendesha shughuli zake hizo kwa muda wa zaidi ya thuluthi karne sasa. Ofisi hiyo ilianzishwa kwa juhudi za pamoja za Mashahidi Murtadha Muttahari, Bahonar na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.402096
captcha