IQNA

‘Atlasi ya Historia ya Kiislamu’ katika maonyesho ya vitabu Tehran

23:31 - May 10, 2009
Habari ID: 1776598
‘Atlasi ya Historia ya Kiislamu’ ni kati ya athari muhimu za kielimu na kihistoria za Taasisi ya Kijiografia ya Jeshi la Iran zinazoonyeshwa katika maonyesho ya 21 ya kimataifa ya vitabu Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika maonyesho hayo, atlasi hiyo imewahi kutunukiwa zawadi ya kitabu cha mwaka cha Jamhuriya Kiislamu ya Iran na vile vile zawadi ya kimataifa ya kitabu cha mwaka duniani.
Atlasi hiyo ni athari ya kipekee na yenye thamani kubwa kwa mtazami ya mpangilio na chapa.
Atlasi ya Historia ya Kiislamu inauzwa kwa bei ya dola 45 katika maonyesho ya vitabu ya Tehran. 402756
captcha