Kwa mujibu wa Tunisian Online News, picha za misikiti na sehemu mbalimbali za ibada za mji wa Qairawan pamoja na miji mingine ya nchi hiyo, zinazochukuliwa kuwa sanaa ya Kiislamu zitaonyeshwa katika maonyesho hayo. Maonyesho hayo yatawasilisha sura halisi ya usanifu majengo wa Kiislamu ambao umekuwa ukitumika kujenga misikiti na maeneo mbengine ya ibada nchini Tunisia tokea karne ya saba hadi leo. Picha za Msikiti Mkuu wa Qairawan uliokarabatiwa katika karne ya nane kwa mbinu ya usanifu majengo wa Kiislamu pia zinaonyeshwa katika maonyesho hayo. 402681