IQNA

Hotuba za Imam Khomeini (SA) zachapishwa kwa Kiarabu

13:06 - May 14, 2009
Habari ID: 1777341
Jildi 22 za Sahifa ya Imam Khomeini (SA) imefasiriwa na kuchapishwa kwa lugha ya Kiarabu na kusambazwa katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayoendelea mjini Tehran.
Sahifa hiyo inajumuisha athari zenye thamani za mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (SA). Athari hizo ni ambazo ni pamoja na hotuba, risala, mahojiano, fatwa , miongozo ya kidini nana barua za Imam Khomeini (SA) zimekusanywa na Tassisi ya Kukusanya na Kueneza Athari za Imam Khomeini (SA). Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammad Moqaddam Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika taasisi hiyo amesema Imam Khomeini (SA) aliweza kuleta mwamko wa Kiislamu na kuuleta Uislamu katika medani ya kisiasa na kufanikiwa kuanzisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran. Mmoja kati ya wafasiri wa wa Sahifa hiyo kwa lugha ya Kiarabu, Munir Masoud amesema misimamo ya kimapinduzi na kishujaa ya Imam Khomeini (SA) inapaswa kupongezwa na kwamba hadi sasa hakuna kiongozi wa Kiarabu aliyeweza kuwa na misimamo imara kama ya Hayati Imam. 403676





captcha