IQNA

Mafunzo maalumu kwa walimu wa Qur'ani nchini Pakistan

11:20 - May 13, 2009
Habari ID: 1777774
Duru maalumu za mafunzo ya usomaji Qur'ani na tajweed maalumu kwa walifu wa Qur'ani zilianza kutekelezwa jana Jumanne huko Islamabad mji mkuu wa Pakistan.
Walimu hao ni wale wanaojishughulisha katika vituo vya mafunzo ya Qur'ani na yatajumuisha usomaji Qur'ani na kusoma kwa mbinu ya tajweed aya za kitabu hicho kitakatifu. Mmoja wa walimu atakayeshiriki katika utoaji masomo hayo ambayo yanafanyika katika Kituo cha Qur'ani cha Jamiatul Mustafa nchini Pakistan ni Abrar Hussein, msomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Pakistan. Mbali na masomo hayo, usomaji Qur'ani wa kila siku utakuwa ukifanyika katika kituo hicho. Masomo hayo yamepangwa kwa namna ambayo yanawawezesha wanafunzi, wanachuo na hata wafanyakazi kushiriki katika masomo bila ya kuathiri shughuli zao nyingine za kila siku, na wakati huohuo kuwawezesha kusoma na kuhifadhi kitabu hicho katika kipindi cha miezi kadhaa. Masomo mengine ya Kiislamu, kama vile tafsiri, fiqhi na sarufi na nahau pia yatatolewa kwa walio na hamu ya kuyasoma. 404013
captcha