Kwa mnasaba wa kuwadia siku za kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatuma Zahra (as), televisheni ya satalaiti ya Ahlul Beit (as) inarusha hewani vipindi maalumu chini ya anwani, 'Nuru katika Maisha ya Zahra (as).'
Vipindi hivyo vinapeperushwa hewani kila siku kuanzia saa 12 kwa wakati wa mji mtakatifu wa Makka, ambapo maulama na watafiti mbalimbali wa Kishia pamoja na mahatibu watazungumzia masuala mbalimbali kuhusiana na maisha na shakhsia inayong'ara ya Bibi Fatma katika Uislamu. Katika sehemu ya kwanza ya vipindi hivyo maalumu, ambayo ilipeperushwa hewani hapo jana Jumanne, Adil bin al-Haj Aal as-Sheikh, mwanafikra mashuhuri wa Syria alizungumzia fadhila na maadili bora na ya kupigiwa mfano ya Bibi Zahra (as). 403896