IQNA

Maonyesho ya michoro kuhusu Sala mjini Istanbul

16:18 - May 14, 2009
Habari ID: 1778335
Maonyesho yenye maudhui ya Sala yamefanika mjini Istanbul Uturuki katika Taasisi ya Misaada ya Birlik.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uturuki, maonyesho hayo yalikuwa na michoro 42 ya rangi katika mafuta. Michoro hiyo imetayarishwa na Arif Urgun, mchoraji maarufu wa Uturuki.
Kati ya maudhui zilizo katika taswira hizo ni pamoja na sala katika medani ya vita, sala wakati mgonjwa akiwa hospitalini na sala katika theluji. 404788
captcha