IQNA

Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran atoa wito kwa Waislamu kuungana

18:57 - May 15, 2009
Habari ID: 1778583
Hatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ametoa wito kwa Waislamu kote duniani kuungana
Ayatollah Imami Kashani ameongeza kuwa, maadui daima wako katika mikakati ya kupanga njama dhidi ya Waislamu. Amesema viongozi wa Marekani na Utawala wa Kizayuni pamoja na waitifaki wao wameweka matumaini yao katika kuibua hitilafu miongoni mwa Waislamu. Ameendelea kusema kuwa maadui hao ndio wanaozusha mifarakano baina ya Mashia na Masunni lakini kutokana na kuwepo umoja wa Waislamu, njama zao hizo zitaambulia patupu.
Akihutubia waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatollah Kashani amesema leo ulimwengu unashuhudia namna mfumo wa Kiislamu wa Iran ulivyopata nguvu na heshima. Amesema madola ya Magharibi na baadhi ya viongozi vibaraka wa nchi za Kiarabu wana wasi wasi kutokana na kuenea kwa kasi Uislamu ulimwnguni. Amesema, maadui hao wametambua kuwa walimwengu wamevutiwa na Uislamu na kwamba mfumo wa Kiislamu ni pigo kubwa kwa satua yao.
Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameashiria safari ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Kurdistan, magharibi mwa Iran na kusema, utawala dhalimu wa mfalme Shah Pahlavi uliwakandamiza Wakurdi kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu. Ameongeza kuwa, hivi sasa chini ya kivuli cha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, wananchi wote wa Iran wameweza kupata heshima na ustawi. Ayatollah Imami Kashani vile vile ameashiria uchaguzi ujao wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utakaofanyika tarehe 12 Juni. Amesisitiza kuwa kushiriki kwa wingi wananchi katika upigaji kura kutatoa pigo kwa njama za maadui dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.405446




captcha