Kwa mujibu wa shirika la habari la As'watul Iraq, polisi ya Iraq imesema kuhusiana na suala hilo kwamba, baadhi ya makundi ya kiwahabi yenye misimamo ya kupindukia yalikuwa na la lengo la kuingiza nchini Iraq vitabu hivyo kwa madhumuni ya kuchochea fitna na mifarakano ya kimadhehebu miongoni mwa Waislamu wa Kishia na Kisuni nchini. Polisi ya Iraq imeongeza kuwa, vitabu hivyo vilivyo na maneno makali ya kichochezi na ya kuzusha ghasia na hata mauaji dhidi ya Mashia, na ambavyo vilikuwa vikiingizwa nchini Iraq kwa anwani ya madawa, viliweza kunaswa na askari usalama wa Iraq baada ya kugundua kuwa vilikuwa vimefichwa katika sanduku moja lililokuwa limefunikwa kwa ustadi mkubwa. Polisi ya Iraq imetangaza kuwa uchunguzi wa mwanzoni unaonyesha kuwa vitabu hivyo vilikusudiwa kupelekwa katika mkoa wa Swalahu Deen na kwamba uchunguzi zaidi ungali unafanyika ili kutambua watu waliotuma na waliokusudiwa kuvipokea vitabu hivyo vya kichochezi dhidi ya Mashia wa Iraq. 405720