Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kongamano hilo la siku mbili limemalizika tarehe 16 Mei katika mji wa Almatu nchini Kazakhstan ambapo washiriki wamejadili masuala mbali mbali ya maadili na siasa katika fikra za kifilosofia za Farabu. Aidha wamejadili kuhusu Farabi na mahitaji ya dunia ya sasa.
Wasomi walioshiriki katika kongamano hili walikuwa kutoka nchi za Iran, Russia, Tajikistan, Kazakhstan na Uzbekistan.
Farabi ambaye jina lake kamili ni Abu Nasr Muhammad ibn Muhammad ibn Tarkhan ibn Awzalagh al-Farabi ,alikuwa msomi bingwa wa Kiislamu aliyezaliwa mwaka 257 Hijria Qamariya (870 Miladia). Alizaliwa katika eneo la Khorassan ya kale lililokuwa sehemu ya wa Iran ambalo leo ni Kazakhstan. Alikuwa kati ya wanafalsafa wakubwa wa Kiislamu katika zama zake. Aidha alikuwa mtaalamu wa mantiki, muziki na sayansi ya siasa. 406432