IQNA

Jumuiya ya Mashirika ya Kiislamu kubuniwa

11:06 - May 19, 2009
Habari ID: 1780342
Wajdi Ghuneim, mwanzuoni mashuhuri wa nchini Misri amesema kuwa kuna wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu wanaojadili mapendekezo kadhaa kwa lengo la kubuniwa jumuiya ya mashirika ya Kiislamu ili kuimarisha miradi ya uchumi wa Kiislamu, kuongeza miamala ya kibiashara na kiuchumi miongoni mwa mashirika ya Kiislamu na kuyasaidia matabaka ya watu masikini katika nchi za Kiislamu.
Kwa mujibu wa shirika la Islamonline, makao makuu ya jumuiya hiyo yatakuwa mjini Brussels, Ubelgiji. Wajdi amesema kuwa lengo kuu la kubuniwa jumuiya hiyo ni kuyasaidia mashirika ya kibiashara na kiuchumi ya Kiislamu kupata kirahisi masoko ya bidhaa zao katika ngazi za kimataifa na kuyawezesha pia kushindana na mashirika ya uzalishaji bidhaa kutoka nchi nyingine za dunia. Malengo mengine ni kuyasaidia matabaka ya watu masikini katika jamii na nchi za Kiislamu kupitia kuanzishwa kwa miradi modogomidogo ya kibiashara kwa familia za wasiojiweza kifedha, kuwalea watoto yatima na wasio na walezi, kuwawezesha wanachuo wa Kiislamu kusoma kwenye vyuo vikuu bora zaidi duniani, kuzisaidia kifedha taasisi za utafiti za Kiislamu, kuunga mikono maeneo matakatifu ya Kiislamu na hasa Msikiti wa al-Aqsa na vilevile wahanga wa mashambulio ya Maghasibu wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 406931
captcha