Ofisi ya Sheikh Hassan as-Swaffar, mwanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini Saudi Arabia ambaye pia ni Imam wa Ijumaa wa mji wa Qatif jana Jumatatu ilitoa taarifa ikiwatumia salamu za rambirambi wananchi wa Iran na umma mzima wa Kiislamu kwa mnasaba wa kuaga dunia Ayatullahil Udhma Muhammad Taqi Bahjat, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu.