Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya masomo katika Chuo Kikuu cha Jamiatul Mostafa (SAW) al Alamiya, wanachuo wasio Wairani waliopata shahada ya kwanza katika vyuo vya kidini wanaweza kujisajilisha kwa ajili ya Shahada ya Uzamili.
Katii ya masomo ya Shahada ya Uzamili ni pamoja na: Fasihi ya Quran, Dini za Nabii Ibrahim, Uchumi, Kuwafahamu Ahlul Bayt, Historia ya Ushia. Erfani na Usufi, Sayansi ya Malezi, Sayansi ya Hadithi, Sayansi ya Siasa, Fiqhi ya Uchumi, Fiqhi ya Mahakama, Filosofia ya Kiislamu, Masomo ya Kijamii n.k.
Wanaotaka kujisajilisha wanaweza kupata fomu katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Jamiatul Mostafa (SAW) al Alamiya inayopaswa kuandamana na picha ya pasipoti pamoja na vyeti vya shahada ya kwanza na masomo menginyeyo.
Muhula wa kujisajilisha ni 12-19 hadi tarehe
Wanaokusudia kujisajilisha wanaweza kupata maelezo zaidi katika tovuti ifuatayo:
http://svp.miu.ac.ir/
407656