Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mtengeneza filamu Muraqi ajulikanaye kama Qasim ambaye filamu aliyotengeneza hivi karibuni, Al Mughni, imekamilika nchini Ufaransa, amesema sasa yuko tayari kutengeneza filamu kuhusu Imam Hussein (AS) katika mji wa Basra kusini mwa Iraq.
Amesema filamu hiyo itatengenezwa kwa ushirikiano na wawekezaji wa kigeni na kuongeza kuwa atashirikiana na watengeneza filamu wa Syria na Misri katika kazi yake hiyo. 408411