IQNA

Kutambuliwa mbinu za maadui, sisitizo muhimu la Kiongozi Muadhamu huko Kurdestan

19:08 - May 22, 2009
Habari ID: 1781158
Nukta muhimu aliyoibainisha Ayatullahil Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduziya Kiislamu ya Iran alipokuwa katika safari yake ya hivi karibuni ya siku nane huko katika Mkoa wa Kurdestan ni kutambuliwa njia na mbinu zinazotumiwa na maadui wa Uislamu na kisha kutahadhari nazo.
Hayo yamebainishwa na Mustafa Ranjabar Shirazi, Mwambata wa Kiutamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania katika mazungumzo yake ya simu na shirika la IQNA. Akitathmini safari hiyo ya Kiongozi Mudhamu, Ranjbar amesema kuwa katika mazingira magumu ya hivi sasa ambapo maadui wa Uislamu wanafanya kila njama ili kuwatenganisha Waislamu, na hasa kwa kutilia maanani kwamba Imam wa Msikiti Mtukufu wa Makka asiyeelewa lolote katika Uislamu, alichukua hatua ya kuwakufurisha Mashia na kuhalalisha damu yao, Kiongozi Muadhamu aliamua kufanya safari katika Mkoa wa Kurdestan nchini Iran, ambao kimsingi ni mkoa wa wafuasi wa madhehebu ya Sunni, na kuhubiri umoja kati ya Waislamu wa madhehebu zote na hivyo kuvunja njama za kutaka kuwatenganisha Waislamu na wakati huohuo kuimarisha nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa kuzingatia kwamba mkoa huo uko katika mpaka wa Iran na Iraq, na ambao tokea mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu umekuwa ukitumiwa vibaya na maadui wa nje na ndani wa mfumo wa Kiislamu katika kujaribu kuvuruga usalama wa Iran na kutaka kuutenga mkoa huo na ardhi yote ya Iran, Ranjbar amesema kuwa safari muhimu ya Kiongozi Muadhamu katika mkoa huo, ambapo alikutana na kuzungumza na matabaka mbalimbali ya wenyeji wa mkoa huo wakiwemo wanazuoni, wanafikra, wasomi, wanachuo na watu wa kawaida na wakuu wa mkoa, imevunja njama zote za maadui za kutaka kuvuruga amani na usalama wa mkoa huo. Muambata huyo wa kiutamaduni wa Iran nchini Tanzania amesema kuwa safari hiyo na maneno ya kuwatia moyo na kuwasifu Wakurdi aliyoyatoa Kiongozi Muadhamu, ni jambo ambalo limewafurahisha mno Wakurdi na kuwafanya wauhudumie hata zaidi mfumo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 407872
captcha